1Wakorinto 9:24-26
Tunahitaji
kupiga mbio za kiroho ili kuliishi kusudi la Mungu ili tuweze kupokea
taji.
Mkristo au mwamini unatakiwa kuishi maisha yanayolenga shabaha katika
kusudi la Mungu ili uje kupokea taji.huwezi kufika mahala bila kuw mpinzani
Waefeso 1;11
Kusudi
ndilo linalosabisha uwepo mahali ulipo,pasipo kusudi la Mungu
usingekuwepo.Mungu anathamini kusudi kuliko maisha,Mazingira unayopitia anaweza
kukuinua ili kuonesha kusudi la Mungu kwa watu.
Wafilipi 3:6-12
Yeremia 1:4-8
Kusudi
linabeba hatima ya maisha yakona kusudi ndilo limebeba ramani ya maisha yako
haijalishi unakataliwa na watu,wala kukutenga ila ni katika kusudi
la Mungu kutimia na kujidhihirisha katika maisha yako.
Isaya 49;1-3
NAWEZAJE KUPIGA MBIO ZA
KIROHO KATIKA KULIISHI KUSUDI LA MUNGU?
UFAHAMU WA KIMUNGU NDANI
YAKO
Kuwa na ufahamu wa kimungu
katika maisha yako kujenga mahusiano yako vizuri na Mungu kunaweza
kukufanya kuishi katika malengo na kusudi la kimungu ndani yako.Bidii yako
katika kusoma neno la Mungu na kukaa vizuri na Mungu itakupa kujitambua.
Isaya 55:10-11 ,Yoshua 1;8
KUJIKANA NAFSI YAKO
Kuacha mambo ambayo
yanakufanya ushindwe kutimiza kusudi la Mungu kwa kupenda kitu fulani
kinachoujaza moyo wako unatakiwa kuyaacha na kujenga mahusiano yako vizuri na
Mungu
KUJITOA MHANGA
Kujitoa kwa kila kitu
katika kumtumikia Mungu kw mali,moyo,akili,na mengineyo kwwa ajili ya kujenga
ufalme wa mungu
No comments:
Post a Comment