Ndani
ya JINA lake kuna Roho KUU itendayo kazi ndani Yetu. Efeso 3:20 “Basi atukuzwe
yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo,
kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; ” Ipo NGUVU INAYOTENDA KAZI NDANI
YAKO, itakayo kuwezesha kufanya Mambo sawa sawa na kwa USAHIHI kama unaitika
katika hilo JINA.
Kama
unayo hiyo ROHO ambayo inakuja kwa Kulijua JINA LA BABA itakusaidia kutenda
Mambo kwa USAHIHI na watu Watakushangaa kwa maana utakuwa UNAPOONGEA au KUFANYA
jambo lolote linakuwa ni la KUELEWEKA.
Kama
unalo JINA LA BWANA, ROHO wa Mungu atatenda Kazi ndani yako. Zaburi 51:10 “Ee
Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. ” JINA LA
BABA linaweka Makao ndani ya mtu aliye SAFI na siyo mtu MUOVU au MUONGO, kama
unataka Kulibeba hilo JINA hakikisha unaishi maisha MATAKATIFU.
Mathayo
5:8 “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. ” Kama unataka kuwa na
hilo JINA hakikisha unaishi katika UTAKATIFU ili kwamba upate kwa NGUVU za ROHO
Mtakatifu ili chochote ukifanyacho unapata matunda na utaishi kwa KUFAIDIKA na
si kuaibika.
No comments:
Post a Comment